A.1 — Hisa za Kuanza na Mwanachama Mpya
K-001
Uanachama unaanza kwa kulipa Hisa za Kianzio — sasa ni Hisa 6 × TSh 50,000 = TSh 300,000. Hizi si ada ya kiingilio bali ni Hisa za kwanza za mwanachama. Mwombaji ana siku 28 tu kulipa kwa mkupuo mmoja. Siku 28 zikipita bila malipo, nafasi inabatilishwa.
K-002
Mwombaji aliyepitishwa anapewa nafasi wazi ya siku 28 kulipa Hisa za Kuanza kamili. Ikiwa hajalipa ndani ya siku 28, nafasi yake inafutika na atalazimika kuomba upya. Idadi ya Hisa za Kuanza inaweza kubadilishwa na Mkutano Mkuu kwa 75%.
K-003
Wanachama waanzilishi 10 wote wana Hisa 6 za kuanza kila mmoja (TSh 300,000 kila mtu) kuanzia 28 Machi 2026.
A.1b — Kanuni ya Kura Moja (One Member, One Vote)
K-004
Kila mwanachama hai ana kura moja (1) tu katika maamuzi yote ya kikundi — bila kujali idadi ya Hisa zake. Mwenye Hisa 6 na mwenye Hisa 100 wana nguvu moja sawa ya maamuzi. Hisa zinatumika kwa Gawio na dhamana tu.
K-005
Vikwazo pekee vya kupiga kura: (a) mwanachama kuwa katika kipindi cha majaribio (miezi 3 ya kwanza), (b) kusimamishwa rasmi, au (c) kuwa na ukinzani wa maslahi katika jambo linalopigiwa kura.
A.2 — Hisa za Kila Mwezi
K-017
Kila mwanachama atachangia angalau Hisa mbili (2) kila mwezi (= TSh 100,000 kwa sasa). Mwanachama anaweza kuweka Hisa zaidi bila kikwazo.
K-006
Hisa zote zimegawanywa 50/50: 50% ni Hisa Huru (dhamana ya mkopo wa mwanachama), 50% ni Hisa za Uwekezaji (uwekezaji wa pamoja — HAZIINGII kama dhamana ya mkopo wa mtu).
K-007
Hisa za Uwekezaji (50%) HAZIWEZI kutumika kama dhamana ya mkopo wa mtu yeyote. Ni nguzo ya ukuaji wa pamoja wa kikundi.
K-008
Tarehe ya mwisho ya michango yote ni siku ya 28 ya kila mwezi. Malipo yanayofika baada ya tarehe hii yatachomeka faini ya 20% mara moja.
A.3 — Ada ya Uendeshaji
K-009
Kila mwezi mwanachama atalipa Ada ya Uendeshaji wakati wa kulipa Hisa zake. Kiwango kitaamuliwa na Mkutano Mkuu kwa kura nyingi.
K-010
Ada ya Uendeshaji itaingizwa kwenye mfuko wa uendeshaji peke yake — tofauti kabisa na mfuko wa Hisa na uwekezaji. Haihesabiwi kama Hisa wala hairudishwi.
K-011
Mhasibu Mkuu atatoa ripoti ya matumizi ya mfuko wa uendeshaji kila robo mwaka.
A.4 — Sifa za Mwanachama Hai
K-012
Mwanachama anaitwa "Hai" anapokidhi SIFA ZOTE: (a) anachangia Hisa 2+ kila mwezi bila kukosa zaidi ya miezi 2; (b) analipa Ada ya Uendeshaji; (c) hana malimbikizo ya faini; (d) anahudhuria vikao; (e) ameweka taarifa ya mrithi wake.
K-013
Mwanachama "Si Hai" hatapiga kura katika maamuzi ya fedha au kiuongozi, wala kugombea nafasi — hadi sifa zake zirejeshewe.
K-014
Kila mwanachama LAZIMA asajili mrithi wa kisheria kwa Katibu ndani ya miezi 2 ya kujiunga.
K-015
Mwombaji wa uanachama lazima aletwe na Mwanachama Mhakikishaji — mwanachama hai anayemjua vizuri, si tu kujuana tu.
K-016
Wajibu wa Mhakikishaji: ikiwa mwanachama aliyemhakikishia ataonekana na dosari ya maadili au udanganyifu ndani ya mwaka mmoja, Mhakikishaji atapitiwa na uongozi.
A.5 — Mahudhurio
K-017b
Mahudhurio ya vikao ni wajibu wa uanachama, si hiari. Mwanachama asiyeweza kuhudhuria atatoa taarifa kwa Katibu kabla ya kikao.
K-018
Kutokuhudhuria bila taarifa inayokubaliwa = faini ya TSh 20,000 inayokatwa moja kwa moja kwenye Hisa. Kutokuhudhuria vikao 3 mfululizo bila sababu = suala linashughulikiwa na uongozi.
A.6 — Tabia Katika Vikao
K-019
Kila mzungumzaji ataomba ruhusa kwa Mwenyekiti. Lugha ya vikao: Kiswahili. Simu za mkononi: lazima ziwe kimya (silent) ndani ya kikao.
K-020
Uamuzi wowote uliofikiwa kwa akidi inayohitajika ni wa mwisho kwa kikao hicho. Hauwezi kufunguliwa tena bila mchakato rasmi wa mabadiliko.
A.3b — Mchango Maalumu (Special Levy)
K-021
Mchango Maalumu HAUKUKUSANYIKI bila: (1) Pendekezo rasmi la maandishi, (2) Taarifa kwa wanachama WOTE si chini ya siku 14, (3) Kikao chenye akidi kamili, (4) Kura ya 2/3 ya wanachama WOTE, (5) Kumbukumbu rasmi kwenye minutes. Mwanachama ana haki ya KUKATAA bila adhabu.